Jumatano, 8 Juni 2016

Umuimu wa fasihi ndani ya jamii

2.3 UMUHIMU YA FASIHI SIMULIZI KATIKA KIPENGELE CHA SEMI (METHALI) KATIKA JAMII HII YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA.
Kwa kutumia methali za Kiswahili zilizoandikwa kwa lugha ya Picha,Tashihisi, Onomatopea/tanakali sauti na methali  za kabila la kisukuma zenye maudhui sawa katika kila methali ya lugha ya kiswahili  kuonyesha nafasi ya utanzu huu katika jamii hii ya sayansi na teknolojia kama ifuatavyo;
 
 Methali ya kisukuma;Gutu gudakilaga ntwe.
 
 Maana;Sikio halizidi kichwa.
 
 Methali yaKiswahili; Mkuza pezi ni papa nyama wote wangawako/nyama wote wangawako mkuza pezi ni papa
 
Ufafanuzi; Methali hizi ni moja na inategemeana na wewe unavyoweza kuanza kuanza au kuandika.unaweza kuanza na mkuza pezi ni papa nyama wote wangawako,au nyama wote wangawako mkuza pezi ni papa.
 Pezi ni kiungo kilichoko ubavuni na mgogoni mwa samaki,akiwemo papa .kiungo hiki kinamwezesha samaki( papa ) kwenda .
            Katika wanyama wote papa ndiye mwenyewe uwezo wa kukuza pezi .methali hii ni sawa na kusema mkuza pezi ni papa wanyama wote wangalikuwepo (wangawako)wanyama wote mkuza pezi ni papa peke yake (hata kama wanyama wote wangelikuwemo na mwenye uwezo wa kukuza pezi ni papa tu.)
 
Maana; a) Mtu pekee mwenye uwezo wa kufanya jambo miongoni mwa wengine .
            b) Mwenye uamuzi wa mwisho. (Mauya B.A,2008).
 
Umuhimu; Methali hii hutumika pale inapoelezea kuweko na mtu tu miongoni mwa walio na uwezo kwa kufanya jambo ambalo wengine hawawezi kulifanya.mfano hata wangelikuwepo wakuu wote wa nchi mwenye uwezo wa mwisho ni Rais
 
Methali ya kisukuma; Nsuji go mva gugamwiwagwa gulali nsebu.
 


 Maana; Mchuzi wa mbwa hunywewa ungali wa moto
 
Methali ya Kiswahili; Udongo uwahi uli maji.
 
Ufafanuzi; Udongo unaweza kufinyangika vizuri bila ya shida uwapo maji .Ukikauka unakuwa mgumu kufinyangika .kama mtu anataka matokeo mazuri,udongo huo ufinyangwe ungali maji ,yaani uwapo mbichi
 
Maana;Wahi kutatua tatizo kabla halijawa kubwa .kwa mfano,
Tibu maradhi kabla ya kukomaa,au wahi kuzuia jambo kabla ya kuharibika .mkanye mototo akiwa mdogo. (Mauya B.A,2008).
 
Umuhimu;Methali hii hutumika kuwapa nasaha watu wasisubiri matatizo hadi yakue .Aidha, methali hii inawaasa watu wasichelewe kushughulikia tatizo mapema ,kabla mambo hayajaharibika .ujumbe wa methali hii nikuwatanabahisha watu kuchukua tahadhari kabla ya hatari .kwa mfano kutibu maradhi kabla ya kukomaa au kuonya watoto wenye mienendo mibaya wakiwa wadogo kabla hawajaharibika  kama vile kuacha ujeuri, udukozi na ugomvi.
 
Methali ya kisukuma;Omasala adabunagwa nigo.
 
Maana;Mwelevu hashindwi kitu.
 
Methali ya Kiswahili;Kozi mwanamandanda kulala na njaa kupenda.
 
Ufafanuzi;Kozi ni aina ya ndege mdogo ambaye hutaga mayai mengi sana.kiasi kwamba mengine anaweza kuyafanya chakula na kuyala na mengine akayatotoa katika hali hii akilala na njaa anapenda, siyo kwamba hana chakula
 
Maana;Mtu mwenye nafasi na uwezo ,kupata taabu ni matakwa yake .tajiri yoyote halali na njaa , akilala na njaa amependa mwenyewe. (Mauya B.A,2008).
 
Umuhimu; Methali hii hutumika kuwaelezea watu wanaojitosheleza katika kila hali .kwao kupata taabu ni kwa kipenda wanyewe .kwa mfano kama mwanafunzi yuko kwenye shule yenye vifaa vya kutosha ,kutokusoma kwake ni kupenda kwake mwenyewe .kama unataka mchumba katika mazingira yenye wanawake na wanaume wengi ,basi kutokuoa na kuolewa ni kupennda kwako mwenyewe
 
Methali ya kisukuma; Nomolomo agagulaga kaya.
 
Maana; Muongo hachagui kabila
 
Methali ya Kiswahili; Mvungu mkeka.
 
Ufafanuzi; mvungu nisehemu yenye uwazi iliyo chini ya kitu kama vile kitanda ,meza na kiti.mkeka ni kitu kama vile jamvi linaloshonwa kutokana na kili na hutumika kwa kulalia kutandikia chini au kitandani . hapa mvungu umefananishwa na mkeka  kwa maana kuwa ,mkeka ukitandikwa chini unaweze ukaficha kitu na kisionekane , kama vile mvungu ufanyavyo..Ndio maana husema mvungu mkeka,kwani vyote vinaweza kuficha kitu na kisionekane.
 
Maana;Usidharau au jihadhari na sehemu za uficho ,kama vile mvungu kwani panaweza pakawa na kitu kilichojificha kama vili nyoka ,mtu au chochote kile ambacho kinaweza kukuletea madhara ama kile mtu anayesikiliza au kuona kile unachokitenda ukadhani ni siri. (Mauya B.A,2008).
 
Umuhimu;Methali hii hutumika kutoa onyo au kuwashauri watu wenye tabia ya kuropokaropoka ,kufanya au kuleta jambo bila kulichunguza yanayomzunguka au sehemu zenye  uficho kama vile chumbani ambamo mna kitanda .
            Hivyo basi, unapokuwa katika sehemu kama hizo lazima uangalie na uchunguze kwanza kabla hujaropoka au kukaa au kufanya jambo lolote.
 
Methali ya kisukuma;Mashi ga mbili gagakwililaga mkaya
 
Maana;Mavi ya mbuzi hujaa zizini.
 
Methaki ya Kiswahili;Ndondondo si chururu.
 
Ufafanuzi;Ndondondo ni kitu kinacho toka kidogo kidogo,kama vile maji ,mafuta .Wakati chururu ni kitu kinacho toka kwa wingi au mfululizo kwa mara moja .kwa lugha nyepesi ,ni sawa na kusema kuwa kidogokidogo kwa muda mrefu si sawa na wingi kwa mara moja.
 
Maana; a) kupata kitu kidogokidogo Kwa muda mrefu ni bora kuliko kupata kingi kwa mara moja.
            b) Kutumia akiba yako kidogokidogo na kwa muda mrefu ni bora kuliko kutumia akiba yote kwa mara moja, ikiisha utabakia na matatizo au shida. (Mauya B.A,2008)
 
Umuhimu; methali hii hutumika kuwaasa watu wenye tabia ya kufuja mali au kutumia pesa /chakula kwa fujo au kwa wingi, kwamba watumie mali zao kidogokidogo na kwa uangalifu.
 
Methali ya kisukuma;Gwigwa go mbulu mpaga mininga mmato.
 
Maana;Kusikia kwa kenge mpaka damu masikioni
 
Methali ya kiswahili;Kama hujui kufa chungulia kaburi.
 
Ufafanuzi;Kaburi ni shimo la kuzikia mtu aliyekufa .Wakati wa kuzika chungulia kaburi utaona kweli kuna kufa maana unaona mtu anavyozikwa.
 
Maana;kujifunza kutokana na matukio au matendo.Kwa mfano ,kama hujui UKIMWI ,kaangalie wanaougua na ukitaka kufeli angalia mtu anayecheza darasani,asiyetaka kusoma kwa bidii matokeo yake ni kufeli. (Mauya B.A,2008)
 
Umuhimu;Methali hii hutumika pale mtu anaposema au kutoa ushauri kwa mtu ambaye ni mbishi ;anayefanya ajizi na jambo la hatari au linaloweza kumuathiri .Aangalie kwa wale waliofanya ajizi  yaliyowatokea.
 
 Methali ya kisukuma;Uyasesilwe mbeho aditanelwagwa moto.
 
 Maana;Aliyepigwa baridi haitiwi moto.
 
Methali ya kiswahili;Mlilala handingwandingwa mwemacho haambiwi tule.
 
Ufafanuzi;Mlilala linamaanisha mtu aliyelala.kundingwandingwa ni kuwa na njaa au kusikia njaa .handingwandingwa lina maana hana njaa .mwemacho lina maana ya mwenye macho .Methali hii ni sawa na kusema? Aliyelala hana njaa na aliye macho haambiwi tule kwani chakula anakiona.
 
Maana;Asiye hangaika hana tatizo ,na mwenye tatizo haambiwi atatue ,tatzo lake (ataangaika ili alitatue.). (Mauya B.A,2008)
 
Umuhimu;Methali hii huwasema watu wasiotaka kujishughulisha au kujituma ili kujiletea maendeleo. Mtu ambaye hataki kujituma ili ajiletee maendeleo basi achana naye kwani hii ni kwa faida yake na mtu anayetaka maendeleo haambiwi la kufanya ili ajiletee maendeleo .Yeye mwenyewe atahangaika kujiletea maendeleo.
 
Methali ya kisukuma;Kugongola gulu gumala mimbo
.
Maana;Ukimwimbia kiziwi nyimbo unajisumbua.
 
Methali ya kiswahili;Uso wa samaki hausikii viungo.
 
Ufafanuzi;Samaki ni kiumbe kinachoishi ndani ya maji (baharini,ziwani au mtoni).Samaki hata aungweje,uso wake haubadiliki.
 
Maana;a)Mtu asiyebadilika (kitabia).
            b)Mtu asiyeshaurika.
            c)Mtu asiye sikia la mtu yoyote. (Mauya B.A,2008)
 
Umuhimu;Methli hii hutumika kuelezea mtu ambaye ni mgumu kubadilika,hasa katika tabia au mwenendo
 
Methali ya kisukuma;Kushema chonza mpanga ubudale
 
Maana;Kukamua kicheche mpaka ulale kifudifudi.
 
Methali ya kiswahili;Utaka cha uvunguni sharti ainame
 
Ufafanuzi;Uvunguni ni sehemu ya chini ya kitu kama vile meza,kitanda au kiti.Nidhahiri ikiwakitu kimewekwa uvunguni ili kukipata lazima uiname ,yaani usiwe mvivu kuinama.
 
Maana;Ukitaka mafanikio lazima ujitume kufanya kazi. .(Mauya B.A,2008)
 
Umuhimu ;Methali hii huwashauri watu wajitume kufanya kazi
 
 Methali ya kisukuma;Nigo go ng’hala gugashililaga gwi bega.
 
Maana;Mali ya mjinga huisha bila kujua
 
Methali ya kiswahili;Mali bila daftari, hughibu bila habari.
 
Ufafanuzi;Mali ni kitu kinachomilikiwa na mtu na kinaweza kuwa kitu au fedha.Daftari ni kitu kinachowekewe hesabu za kitu au fedha na siku zote mtu makini mali yake, huweka hesabu ya mali yake kwenye daftari. Hii inamsaidia kufuata mienendo ya mali yake ili kuepuka upotevu.
 
Maana;a)mali bila kuwekea kumbukumbu kimaandishi hupotea bila ya habari.
            b)Mara nyingi ,anapata hasara asiyeweka kumbukumbu ya mali yake. (Mauya.B.A,2008)
 
Umuhimu ;Methali hii hutufundisha tuwe tunaweka mali zetu katika kumbukumbu au maandishi
 
 Methali ya kisukuma;Gulya mwa mpanga.
 
Maana;kula ni uhai.
 
Methali ya kiswahili;Ukitaka kula nguruwe chagua aliyenona.
 
Ufafanuzi;Kwa waislamu kula nguruwe ni haramu Kwa mujibu wa dini yake mwislamu kakatazwa kula nguruwe,Inapotokea,kwa makusudi,mwislamu kula nguruwe ,na kuvunja imani hiyo,inaaonekana ni vizuri basi, mtu wa namna hiyo ale nguruwe aliyenona.Haimkini mtu kuvunja imani kwa kula nguruwe aliyekonda kwa kwenda kinyume cha dini.
 
Maana; a) Unapotaka kufanya jambo linaloweza kukuletea madhara,ulifanye kikwelikweli au kwa dhati.
b) Ukitaka kufanya ambo fanya kwa dhati.
            c) Ukiamua kufanya jambo liwe la heri au la shari fanya kwa bidii na nguvu zote (fanya kikwelikweli katika kiwango cha juu). (MauyaB.A,2008).
 
Umuhimu; Methali hii hutumika pale mtu anapoamua kufanya jambo kwa makusudi ,jambo ambalo litamletea madhara ,basi anapaswa kulifanya kwa mafanikio ya hali ya juu.
 
Methali ya kisikuma; Gugulu guli ng’ombe, idako ilalija.
 
Maana; Mtembezi hula miguu yake na mkaaji hulala njaa.
 
Methali ya Kiswahili; Mgaaga na upwa hali wali mkavu.
 
Ufafanuzi; kugaagaa ni kugeukageuka katika hali ya kujilaza. Hapa kugaagaa imetumika kumaanisha kutembeatembea
Upwa ni kandokando ya bahari ambapo maji hujaa na kupwa. Mara nyingi, sehemu kama hizi hupatikana samaki ambao wamesukumwa na maji na kuachwa mchangani
Mgaagaa na upwa ni sawa na kusema hali wali mkavu ni sawa na kusema anaetembeatembea kando kando ya bahari hali wali mkavu, maana anaweza akaokota hata kisamaki au kidagaa na kupata kitowewo.
 
Maana; Anayefanya juhudi katika kazi, masomo au jambo lolota hufanikiwa. (Mauya B.A,2008)
 
Umuhimu; Methali hii hutumika katika kuwahimiza au kuwashauri watu wafanye bidii katika shughuli zao na watafaniliwa. Wasijikalie tu.
 
 Methali ya kisukuma; Gukungila nungu gwelwang’holo
 
Maana; kuwinda nungunungu ni jambo la maana
 
Methali ya Kiswahili;kata  pua uunge wajihi.
 
Ufafanuzi; kata pua uunge wajii ni sawa na kutoa kijinofu cha pua na kukuunga kwenye sehemu nyingine ya uso iliyoharibika iliionekane nzuri. Kwa maana nyingine ni kutoa au kupunguza kitu mahali na kwenda kufidia pengine.
 
Maana; Linda hadhi au heshima yako hatakama itakugalimu . Unaweza kupunguza kiasi fulani cha mali au pesa ili uilinde hiyo heshima kwa mfano kama mtu anakaribiwa na tatizo ambalo kama hatalitatua litamfedhehesha. Mtu mwenye njaa, kesi au deni, ita mbidi, hafanye chini juu au aende mbio, hatakama kuuza au kuweka poni baadhi ya mali zake atatue tatizo hilo ili asihathilike. Anapouza na kuweka poni baadhi ya mali zake ndipo anapokata pua na kuunga wajii yaani kuilisnda heshima. Hii inamaana mtu hawezi kubaki na shida kama anacho kitu ambacho anaweza kukibadili kwa njia yoyote ili atatue hiyo shida. Huwezi ukawa unadeni la kukuathili wakati uacheleani au baiskeli ndani ya nyumba na usiwezw kuuza au kuweka rehani na kutatua tatizo hilo, maana kifaacho mtu ni chake, kata pua uunge wajihi. (Mauya B.A,2008)
 
Umuhimu ; methali hii huwashauri watu watumie malizao au asilimali zao katika kutatua matatizo yao, wasipate taabu wakati wanavyo vitu vya kuwasaidia katika matatizo yao.
 
Methali ya kisukuma; Lubigi lo kule  ludabulagaga.
 
Maana;Fimbo ya mbali haiui
 
Methali ya kiswahili;Hamadi kibindoni silaha iliyo mkononi
 
Ufafanuzi;Hamadi ni neno linalotokana na mahamad(Mtume).pia ni neno linaloonyesha mshtuko au kitendo cha ghafla .Kibindoni ni ndani ya mkunjo wa nguo .kama vile shuka au kikoi ,unaokunjwa mithili ya mfuko na mara nyingi hutumika kuwekea fedha.Hivyo basi kibindoni ni kama mfuko wa kuwekea fedha,kwa maana hiyo basi ,methali hii ni sawa na kusema kwa  jina la muhamad  kuwa na pesa kibindoni ni sawa na kuwa na silaha mkononi pale inapohitajika.hadhari ni mfukoni au kitu ulichonacho .
 
Maana;kuwa na pesa mfukoni ni sawa na kuwa na silaha mkononi pale inapoitajika (mbele ya adui).Pia ni sawa na kusema pale mtu anapopatwa na tatizo lolote kile kitu kitakachokusaidia ni kile kilicho mbele yako;awe mtu ,kitu au kifaa chochote kile .mathalani umepatikana na tatizo na linahitajika kutatuliwa kwa pesa.pesa itakayokusaidia ni ile uliyo nayo hapa hapo ulipo iwe ndani ya mfuko au mkononi,kuliko ile ambayo ipo mahali pengine ,kama vile iliyo benki, nyumbani au kwa mtu mwingine ingawa ni yako.hali kadhalika kama umetokewa na adui yako ghafla silaha itakayo kusaidia ni ile iliyopo mkononi na siyo ile iliyo mahali pengine .
Kwa maana nyingine kitakacho kusaidia ni kile kilichoko mbele yako yaani kile ulichonacho hapohapo kuliko kilicho mbali na wewe .hata ukivamiwa na adui wa kukusaidia ni jirani yako au yoyote yule atakayekuwa karibu yako kwa wakati ule. (Mauya B.A,2008)
 
Umuhimu; methali hii hutoa hadhari kwa mtu ajiwekee akiba au awe na uhusiano mzuri na majirani zake na hajihadhari na lolote na kwa wakati wowote ,yaani asijisahau kila waksti awe amejitayarisha kwa lolote lile.
 
Methali ya kisukuma; kulanga shelangile ukwikumya na bulangi
 
Maana; kufundusha kinachofundishika utajivuna unajua kufundisha
 
Methali ya Kiswahili; kutwanga nisile unga nazuia mchi wangu
 
Ufafanuzi;ni kuponda kitu,kama vile mtama au mahindi katika kinu kwa kutumia mchi ili kutoa punje.Baada ya kutwanga punje huweza kufundwa na kutoa unga wa kula .inapotokea mtwangaji hapati ule unga basi anaweza kukata tamaa kutwanga na hivyo kuzuia mchi wake ,kwa maana hatwangi tena. 
 
Maana; Mtu asipotuzwa au kufaidika kwa kazi anayoifanya anaweza asiendelee kufanya kazi hiyo au mtu asipopata motisha au malipo atapunguza juhudi za kazi au kuacha kabisa kufanya kazi hiyo. (Mauya B.A,2008)
 
Umuhimu; Hutumika kutoa onyo kwa watu ambao hawapendi kutoa malipo/ujira unaostahili kwa aliyefanya kazi au kutoa shukran kwa mtu aliyemtendea mema
 
 
 
 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni